Uhalifu wa kimabavu unazidi kuongezeka nchini Afrika Kusini, huku wizi wa pesa katika magari yanayosafirisha fedha ukiwa jambo la kawaida na kiwango cha mauaji kikiwa juu.
Hali hii inaifanya nchi ya Afrika Kusini kuwa tishio kwa wafanyabiashara na wawekezaji nchini humo.