Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemuagiza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Eng. Godfrey Kasekenya kufika katika maeneo yaliyoathiriwa na mvua mkoani Dar es Salaam na kuungana na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Mohamed Besta, pamoja na timu ya wataalam kuhakikisha wanachukua hatua za haraka kwa kurejesha mawasiliano ya barabara na madaraja yaliathiriwa ili wananchi waweze kuendelea na shughuli zao.
Waziri Bashungwa ameyasema hayo wakati akitoa pole kwa wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kupitia Mkuu wa Mkoa huo, Albert Chalamila kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia jana tarehe 21 Januari, 2024.