Kabir Abu Bilal sio profesa wa kawaida wa chuo kikuu cha Nigeria anayo kazi nyingine ya kuchomelea vyuma kaskazini mwa jiji la Zaria.
Uchomeleaji unaonekana sana kama kazi duni kote nchini Nigeria na amewashangaza wengi hasa wafanyakazi wenzake kwa kufungua karakana yake ya uchomeleaji.
“Ninapata pesa zaidi kutokana na uchomaji vyuma”.
Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 50 anafundisha na kusimamia wanafunzi wa utafiti katika kitivo cha uhandisi katika Chuo Kikuu cha Ahmadu Bello, Chuo kikuu kikubwa zaidi na chenye hadhi nchini Nigeria.