Mtandao wa YouTube umesitisha rasmi chaneli ya kanisa kuu la mwinjilisti wa televisheni kutoka Nigeria TB Joshua kwa kukiuka sera zake za matamshi ya chuki.
Hatua hiyo inajiri wiki kadhaa baada ya kufichuliwa kwa ushahidi wa kuenea kwa unyanyasaji wa kingono na mateso yaliotekelezwa na mhubiri.
Emmanuel TV ilichukua jukumu muhimu katika kuimarika kwake kutoka kuwa mchungaji wa ndani hadi kuwa nyota wa kimataifa.
TB Joshua alifariki mwaka 2021, lakini Kanisa lake la Synagogue Church of All Nations (Scoan) sasa linaongozwa na mkewe Evelyn Joshua.
Chanzo: BBC Swahili