Chama Cha Mapinduzi kimezitaka Taasisi za kibenki ambazo ziliwakopesha Wafanyabiashara wa soko maarufu la Mbuyuni lililopo Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro kuwalipa fidia baada ya soko hilo kuungua kwa moto na kupelekea biashara za Wafanyabiashara zaidi ya 2,500 kuteketea.
Moto huo, unadaiwa kuanza kuwaka majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo Februari 6, 2024 huku chanzo chake kikiwa bado hakijajulikana, na kusababisha hasara kubwa kwa Wafanyabiashara hao ambao asilimia kubwa wamedai walikuwa wakijiendesha kwa mikopo.