Hali halisi ilivyo katika mji wa Goma baada ya kuzuka kwa ghasia na mapigano ambayo yamewasababisha watu zaidi ya milioni saba kuwa wakimbizi wa ndani na kuhama makazi yao kwa sababu ya vita vya mara kwa mara.
Waasi kutoka kundi la M23 ambalo linaongozwa na jamii ya AbaTutsi wamefunga barabara mbili kuu zinazoingia na kutoka Goma kwa upande wa Kaskazini na magharibi na kutatiza hatua za kuingiza chakula mjini humo.