Hayati Edward Ngoyai Lowassa alizaliwa mkoani Arusha tarehe 26/08/1953. Alikuwa waziri mkuu tangu mwaka 2005 – 2008 chini ya uongozi wa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete.
Mwaka 2008 alitangaza kujiuzulu baada ya sakata la Richmond lililompelekea kuchafuka kisiasa na kuamua kuachia madaraka ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Mh. Mizengo Pinda.
Safari yake ya kisiasa ilianza rasmi mwaka 1977 alipojiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) hadi mwaka 2015 alipohamia CHADEMA na baadaye mwaka 2019 akarudi tena CCM mpaka mauti yalipomfika.
Edward Ngoyai Lowassa amefariki tarehe 10/02/2024 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) akiwa na umri wa miaka 70.