Waziri mkuu, Kassim Majaliwa anahutubia wananchi wa Wilaya ya Butiama.
Katika ziara yake Wilayani Butiama Mh. Waziri Mkuu ameongozana na Mbunge wa Jimbo la Butiama Jumanne Sagini, Mkuu wa mkoa wa Mara, Naibu Waziri wa Madini na Waziri wa Maji Mh. Juma Awezo.
Baada ya kuhutubia na kusalimiana na wananchi wa Butiama, Waziri Mkuu ataelekea Serengeti na baadaye wilaya ya Tarime.