Klabu ya Azam FC imempa ofa ya mshahara wa dola 15,000 (zaidi ya milioni 38 za Kitanzania) kwa mwezi na ada ya usajili ya ya milioni 300 mshambuliaji wa kimataifa wa DR Congo na klabu ya Pyramids FC ya Misri, Fiston Kalala Mayele ili asaini mkataba wa miaka miwili mwisho wa msimu.
Mayele ambaye ni Mshambuliaji wa zamani wa Young Africans anadaiwa kuwa ameandika barua kwa klabu yake ya Pyramids FC kuomba kuondoka na iwapo atakubaliwa huenda akajiunga na Azam FC kuchukua nafasi ya Mshambuliaji Prince Dube raia wa Zimbabwe aliyeondoka Azam FC baada ya kuandika barua ya kuvunja mkataba na klabu hiyo mapema mwezi huu.