Ndege binafsi ya P Diddy, imefuatiliwa hadi visiwa vya Antigua huku polisi wakivamia makazi yake ya Los Angeles na Miami, na wanawe Justin na King wakikamatwa.
Ndege ya Gulfstream 5 ilifanya safari kadhaa ndani ya California kabla ya kuelekea huko Antigua ingawa haijulikani kama P Diddy
mwenyewe alikuwepo ndani ya ndege hiyo.
Taarifa rasmi kutoka kwa wawakilishi wa P Diddy ama timu ya wanasheria wake bado haijatolewa juu ya sakata hilo na hata P Diddy mwenyewe mpaka sasa hajulikani alipo na msako wa ‘nyani’ unaendelea.