Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Mhe, Samia Suluhu Hassan leo Machi 31, amegawa pikipiki kwa Viongozi wa Chama ngazi ya Kata na jumuiya zote Wilayani Butiama.
Akiongoza zoezi hilo, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Butiama Mhe, Christopher Siagi amesema Pikipiki hizo zitaenda kurahisisha shughuli mbalimbali za chama kwa urahisi na ufanisi mkubwa.