Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Paul Christian Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Kabla ya uteuzi huo, Makonda alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Taarifa iliyotolewa usiku wa kuamkia leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella atapangiwa nafasi nyingine.
Rais Samia pia amemteua Kanali Evance Mtambi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Aidha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Said Mtanda amehamishwa kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, akichukua nafasi ya Amos Makalla ambaye atapangiwa kazi nyingine.