Kampuni ya simu za mkononi ya Infinix Mobile Tanzania imezindua rasmi toleo jipya la simu za NOTE 40 series na kutangaza kuwa sasa ni rasmi simu hizo zimeanza kuuzwa Nchini Tanzania.
Moja ya sifa kuu za simu hizo imetajwa kuwa ni teknolojia ya kuchaji wa haraka iitwayo All Round Fast Charge 2.0, watt 70 ambayo ina uwezo wa kuchaji kwa haraka na kufikisha asilimia 50 ndani ya muda wa dakika 16 tu ambapo pia toleo la NOTE 40 pro limekuja na teknolojia ya wireless charge yenye Watt 20 ambayo inampa Mtumiaji urahisi wa kuchaji anapokuwa mihangaikoni pasipo kutumia wire kama kauli mbiu yao inavyosema #Takecharge247
Infinix NOTE 40 Series imetengenezwa kwa umahiri na chip cheetax X1, chip ambayo imetengenezwa na Infinix wenyewe ili kuongeza ufanisi katika teknolojia hii ya fast charge ambapo kwa upande wa picha camera yake ni ya megapixel 108 pamoja na kuzoom kwa usaidizi wa OIS na umbo lenye muundo wa kisasa wa 3D Curved, AMOLED Display na refresh rate 120Hz.
Katika uzinduzi huo, Infinix imetangaza kuwa sasa NOTE 40 series zipo madukani Nchini Tanzania ambapo wamewaongezea Wateja wa simu hizo ofa ya GB 96 za internet kutoka Vodacom na nafasi ya kwenda nje au ndani ya Nchi kwa kutumia usafiri wa ndege ya Air Tanzania (ATCL) “tunawakaribisha Wateja wetu kutupigia simu kupitia 0656317737/ 0743558994 kwa maulizo mbalimbali”.