Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya basi la Lujiga Express lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza lenye namba za usajili T 315 CXX iliyotokea wilayani Iramba mkoani Singida imefikia 9 na majeruhi 19.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba Daniel Paul amesema kati ya majeruhi hao, watatu ambao walilazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba (Kiomboi) alikuwepo mwanamke mjamzito ambaye baada ya kufanyiwa operesheni wamekuta mtoto amefariki tumboni.
Ajali hiyo imetokea leo Aprili 10, 2024 majira saa kumi na moja alfajiri basi la Lujiga Express liligonga lori kwa nyuma lililokuwa limeengeshwa barabarani baada ya kuharibika katika kijiiji cha Mseko mkoani Singida.