Mwanafunzi mmoja amepoteza maisha na saba hawajulikani walipo baada ya gari la shule ya Msingi Ghati Memorial, iliyopo Mkoani Arusha, kuanguka kwenye korongo linalopitisha maji.
Ajali hiyo imetokea katika mitaa ya dampo Sinoni, Kata ya Muriet huku chanzo kikidaiwa kuwa ni dereva wa gari hilo kushindwa kulidhibiti, kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.