Taarifa iliyosambaa awali kuwa Mchezaji Rainford Kalaba amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari imekanushwa na madaktari wa hospitali moja huko Lusaka nchini Zambia alikofikishwa mchezaji huyo kwa matibabu ya haraka.
Hospitali hiyo imetoa taarifa kuwa mchezaji huyo amefikishwa hospitalini hapo akiwa na hali mbaya sana ambapo baada ya vipimo vya awali waligundua kuwa hajafariki dunia na kwamba kwa sasa yuko katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU).
Kwa taarifa zaidi endelea kutufuatilia hapa na kwenye mitandao yetu ya kijamii.