Bahari mpya inaibuka barani Afrika, kulingana na utafiti mpya, ni mchakato ambao ulidhaniwa ungechukua kati ya miaka milioni 5 na 10, lakini utafiti mpya wa kisayansi unaonesha kuibuka huko kunaweza kutokea kwa kasi zaidi ya ilivyotarajiwa.
Cynthia Ebinger, mtafiti katika Chuo Kikuu cha Tulane nchini Marekani na profesa wa jiolojia tangu miaka ya 1980, anasema “wakati bahari mpya ilipoanza kuibuka – ilitarajiwa kuchukua mamilioni ya miaka lakini sasa inaonekana itachukua chini ya hapo.’’
Kulingana na tovuti ya Google, Ebinger ameandika zaidi ya makala 16,000 katika majarida ya kisayansi na ndiye mtaalamu anayeaminika katika uwanja wa jiolojia na mazingira duniani.
Mwaka 2023, makala 17 zilichapishwa, zikieleza juu ya mkondo mpya wa bahari utakaoibuka katika eneo la Afar, Ethiopia ambalo liko kwenye mipaka ya nchi hiyo pamoja Eritrea na Djibouti.
Credit: BBC Swahili