Klabu ya soka ya Yanga leo imecheza mchezo wake wa 26 dhidi ya Kagera Sugar ambapo katika mchezo huo Yanga imepata pointi tatu kwa kufunga goli moja kupitia kwa mchezaji wao, Mudathir Yahya aliyeingia kipindi cha pili.
Mpaka sasa Yanga imebakia na michezo 4 ikiwa imevuna jumla ya pointi 68 juu ya watani wao Simba SC ambao wamebakia na michezo 5 wakiwa na jumla ya pointi 53 huku Azam FC wakiwa nafasi ya pili na pointi 57.
Huu hapa Msimamo wa Ligi kuu ya NBC 2024
![](https://www.togoromedia.co.tz/wp-content/uploads/2024/05/IMG_20240508_221915-527x1024.jpg)