Katika kukabiliana na Wanyamapori hususani Mamba na Kiboko, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Nchini – TAWA, Kanda Maalum ya Dar es Salaam imewapa mafunzo maalum Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Zimbwini, iliyopo Kibiti Mkoani Pwani.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Afisa Mhifadhi wa Mamlaka hiyo, Sanjo Mafuru amesema uamuzi wa kuendeshani kwa ajili ya kuwaelimisha Wanafunzi wanaoishi katika jamii zinazozunguka maeneo yanayoashiria uwepo wa Wanyamapori hao.
Amesema, “ili kujihami na kujilinda na Mamba uvukapo mto au anapopita kwenye maeneo yenye mamba hakikisha una mti au fimbo yenye ncha Kali na iwapo atakuvamia mchome kwenye macho au kichwani kwa kutumia fimbo au mti huo wenye ncha Kali, iwapo huna kitu chenye ncha Kali tumia hata vidole vyako kumtoboa mamba kwenye macho yake naye atakuachia.”