Watu watatu mkoani Geita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumteka mtoto mwenye umri wa miaka minne na kuitaka familia ya mtoto huyo kuwapatia Shilingi Milioni 4 ili waweze kumwachia huru mtoto huyo.
Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Bi.Safia Jongo , amesema tukio limetokea huko wilayani Mbogwe, na kwamba watekaji hao walitoa siku nne wawe wametumiwa fedha hizo, lakini Jeshi hilo limepambana na kufanikiwa kuwakamata ndani siku tatu
Chanzo: ITV