Tume ya Maendeleo ya ushirika Tanzania imeingia makubaliano na mtandao wa simu wa Tigo kwa lengo la kuongeza ufanisi kwenye vyama vya ushirika Nchini kwa kuboresha mifumo ya mauzo ya mazao ya wakulima.
![](https://www.togoromedia.co.tz/wp-content/uploads/2024/01/AB7354E3-7A14-4508-843B-82DEE2F1C1C0-600x341-1.jpeg)
Akizungumza na waandishi wa habari Mrajisi wa vyama vya ushirika na mtendaji mkuu wa tume ya Maendeleo ya ushirika BENSON NDIEGE amesema mfumo huo umeanzishwa kutokana na uwepo wa changamoto ya ubadhilifu na wizi wa fedha za wakulima hivyo ushirikiano huo utawezesha kulipia kwa mfumo rasmi.
Credit: Bongo 5