Waziri wa nchi ofisi ya Rais menejiment ya utumishi wa umma na utawala bora ,George Simbachawene amezitaka taasisi zote za umma nchini kuhakikisha zinaingia kwenye mfumo wa serikali mtandao( e-GA) ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi unaoendana na sayansi na teknolojia na hatimaye wananchi kuweza kufikiwa na huduma kwa urahisi popote pale walipo.
Ameyasema hayo leo mkoani Arusha wakati akifungua kikao kazi cha 4 cha wadau wa serikali mtandao kinachofanyika kwa muda wa siku tatu mkoani Arusha.
Simbachawene amesema kuwa,ni wajibu wa kila taasisi kuhakikisha inaingia kwenye mfumo huo ili kuwezesha upatikanaji wa huduma kwa wananchi kwa wakati kwani hilo ndo jukumu lao kubwa.