Leo ni ziara ya Mh. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wilaya ya Butiama ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoa wa Mara ambapo anatarajiwa kusalimiana na wananchi wa Butiama katika viunga vya Mwanzo Mwisho Butiama mjini.
Baada ya kusalimiana na wananchi wa Butiama, Mh. Majaliwa ataelekea wilaya ya Serengeti.