Leo Mamelod Sundowns wamewapa Yanga gari bovu ambalo limeharibika baada ya kilometa 5 tu kutoka OR Tambo International Airport, Afrika Kusini.
Ikumbukwe kuwa Mamelod walikataa gari waliopewa na Yanga kuwapokea pale Julius Nyerere International Airport walipowasili nchini kwa mchezo wao wa kwanza wa robo fainali ya CAF Champions League dhidi ya Yanga.