Leo April 12 ni siku ya kumbukizi ya miaka 40 ya kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daktari Samia Suluhu Hassan amefika Jijini humo.
Katika hotuba yake, Mhe. Paul Christian Makonda mbele ya Rais Samia, amesema “Nna ombi dogo…pale katikati ya jiji la Arusha, tuna barabara mbovu sana Mh.Rais….kwa kweli bila mkono wako hatutoki, ningekuomba tu kwa unyenyekevu mkubwa mama yangu mpendwa, na wao kwenye kikao walikuwa wananiambia huyo si mama yako?, nenda… kwa hiyo Mh.Rais hapa napimwa kama kweli wewe ni mama yangu au la“. Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw.Paul Makonda.