Aliekuwa Dj maarufu kutoka Clouds Fm na Clouds TV, Dj. D Ommy ameondoka Clouds Media Group rasmi leo.
D Ommy ameondoka muda mfupi baada ya kutangazwa kujiunga na team mpya ya Jahazi ambapo wengine waliotangazwa Jahazini ni B Dozen na Adam Mchomvu.
Mkuu wa maudhui wa Clouds Media, Bwana Sebastian Maganga amethibitisha taarifa hizo na kusema kuwa pande zote mbili zimekubaliana kufikia maamuzi hayo.